Duration 20:48

MRADI WA UHIFADHI CHANZO CHA MAJI MANG'OLA WAKAMILIKA

114 watched
0
1
Published 16 Aug 2021

#Documentary: Kazi ya utekelezaji wa mradi huu wa UHIFADHI CHANZO CHA MAJI chemchemi za Qang'dend na Mto Mang'ola ndani ya kijiji cha Qang'dend, Kata ya Baray, Tarafa ya Eyasi, Wilaya ya Karatu mkoani Arusha imekamilika kwa asilimia 100. Shughuli zilizofanyika pamoja na mambo mengine ni uwekaji wa nguzo za kudumu za mpaka (beacons) zipatazo 1000, ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji, ujenzi wa birika la kunyweshea mifuko, pampu za kusukuma maji na ujenzi wa Bwawa moja kubwa la kuzuia mchanga vyote vikiwa vimekamilika na mradi umeanza kufanya kazi. Kazi zote za ujenzi katika utekelezaji wa mradi huu zilifanyika chini ya usimamizi wa wataalamu wa Bodi ya Maji Bonde la Kati akiwemo Mhandisi wa Kitengo cha Mazingira na Mhandisi wa ujenzi katika Ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la Kati kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu. Mradi huu mkubwa na wa kihistoria ambao umetekelezwa kwa nguvu ya rasilimali za wataalamu wa ndani "force account" kwa gharama ya Tsh. 478,444,445,- ujenzi wake umekamilishwa ndani ya miezi 5 pekee.

Category

Show more

Comments - 0